- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- redhot@storymojaafrica.co.ke
Katika mkusanyiko huu wa hadithi, mafumbo tata yanafumbuliwa. Katika hadithi ya Nguli wa Kaya siri za kale za uhusiano wa msitu na jamii zinabainika, wakati huo katika Aste Aste tishio la hujuma za kijidijitali zinafichuliwa, ilhali katika Farasi asiye na Farisi ushindani wa viongozi kuleta matumaini na faraja unamulikwa.
Hadithi hizi zinaakisi mada za masuala mtaambuko na maadili zinazompa msomaji na mwanafunzi hamu ya kujiburudisha, kasi ya kusoma, ari ya kuvinjari na uwezo wa kuwa na umilisi. Kupitia msururu huu wa hadithi, msamiati huongezeka, mawazo hupanuka na uzoefu wa mambo unaimarika.