- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- redhot@storymojaafrica.co.ke
Riwaya hii ni ya wanafunzi walio kati ya Gredi ya 7-9.
Mara tu Nairese alipotia mguu wake ndani ya kantini, wanaume wawili kutoka msitu wa karibu walimvamia kwa ghafla. Walimfunga macho na mdomo kwa vitambaa na kumburuta hadi katikati ya msitu mkubwa wa Kaithe, msitu ambao hakuna aliyethubutu kuuingia isipokuwa majasiri na wale majambazi. Nairese alijitahidi kujinasua, lakini wanaume wale walimshinda nguvu. Alikuwa kama nzi kwenye pembe ya ndovu. Watu walipogundua kuwa Nairese hayupo, majangili walikuwa tayari wametoweka ndani ya kina cha msitu. Nairese aatafanya nini ili kuepuke mtego wa ndoa ya mapema? Je, atafanikiwa katika dhamira yake ya kuwa nyota wa jamii yake?