- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- redhot@storymojaafrica.co.ke
“... Wakati wa ukombozi ukifika haukawilishwi. Ukombozi ni
mithili ya mawingu; yashibapo, hayakawii kuiachilia mvua. Huu
ndio wakati tuliomo sasa.”
Jitihada za ukombozi zinahitaji ujasiri wa kukabili mambo ambayo
wengi huyaogopa. Kama ilivyo safari yenye milima na miteremko,
jitihada hizo hukumbwa na changamoto kama kukataliwa na
jamaa na marafiki au hata usaliti. Hata hivyo, mwishowe jitihada
hizo huzaa matunda.
Narudi Nyumbani ni tamthilia yenye mvuto wa aina yake
inayoeleza azma ya mhusika Shani kuizindua jamii na kuikomboa
kutoka kwenye tamaduni hasi. Katika azma yake, anapigwa kumbo
na watu mbalimbali na kupigwa jeki na wengine. Je, Shani
anafaulu katika azma hii? Je, mbona kauli ‘narudi nyumbani’? Ni
nani anayerudi nyumbani? Anarudi nyumbani akitoka wapi?