- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- redhot@storymojaafrica.co.ke
Talii ulimwengu wa kuvutia wa Fasihi ya Kisasa ya Kiswahili kwa kusoma Mke Mwana na Hadithi Nyingine. Huu ni mkusanyo wa hadithi fupi za kusisimua zilizoandikwa na waandishi wenye tajriba pana katika uandishi wa kazi za fasihi. Mkusanyiko huu utakuwezesha kutambua hali ya maisha ya mwanadamu wa kisasa kupitia mandhari za hadithi na maudhui mbalimbali yaliyoshughulikiwa ndani yake kama vile mahusiano, siasa, umaskini, elimu, ufisadi, teknolojia na masuala mengineyo ya kijamii.
Matumizi faafu ya vipengele ya fani kama muundo, mtindo, lugha na wahusika wenye sifa na majukumu mbalimbali ni baadhi ya mambo yatakayokuzamisha ndani ya hisia na uzoefu wa mwanadamu ukisoma hadithi za mkusanyiko huu.