- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- redhot@storymojaafrica.co.ke
Barua ya Mwisho na Hadithi Nyingine ni mkusanyiko wa hadithi fupi zilizoandikwa na waandishi wenye uzoefu mpana wa kuandika kazi za fasihi. Hadithi zilizomo zinaangazia masuala yanayochora taswira kamili ya tajriba ya mwanadamu wa kisasa katika mazingira anuwai.
Matukio yamesukwa kwa njia inayoakisi uhalisia wa maisha ya kila siku ya wanajamii na kuchangia kukemea maovu na kukuza matendo ya kiuadilifu katika jamii kupitia maudhui tofauti tofauti kama vile elimu, siasa, teknologia na madhara yake, ufisadi, ulanguzi wa dawa za kulevya, matatizo ya kiuchumi, mimba na ndoa za mapema, miongoni mwa mengine.
Kunao pia uanuwai na ufaafu wa matumizi ya vipengele mbalimbali vya fani kama vile muundo, mtindo, lugha na wahusika katika mkusanyiko huu. Huu ni mchango mkubwa katika fasihi ya Kiswahili kwenye Karne ya Ishirini na Moja.