- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- redhot@storymojaafrica.co.ke
Katika msuko wa safari ya wakati, Safari na Betty, ambao ni mapacha, wanajipata katikati ya jamii ya Wakasigau wanaoishi kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania,wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia. Kwa vile Wakasigau hawakuweza kuwatofautisha maadui sugu – wanajeshi wa kikoloni wa Uingereza na Ujerumani, wanadaiwa kusaliti mrengo mmoja dhidi ya mwingine. Kutokana na tuhuma ya uhaini, wanahukumiwa kifo. Safari, Betty na familia yao mpya ya Wakasigau wanalazimishwa kufunga safari hatari ambayo inawakutanisha na balaa bin
beluwa kwa kila hatua wanayosonga. Je, mapacha hao watanusurika? Je, Wakasigau wataishi au watanyamazishwa milele?