- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- orders@storymojaafrica.co.ke
Katika mkusanyo huu wa hadithi, utakumbana na matukio usioyatarajia. Katika hadithi ya Simulizi za Utotoni na Usipoziba Ufa... ujirani mwema unatuachia athari katika maisha yetu, wakati huo huo katika Mawimbi ya Mabadiliko changamoto ya kufanya kazi katika mazingira yenye siutafahamu inaangaziwa, ilhalia katika Mtazamo Mpana unahimizwa katikati ya migogoro, na bila shaka katika Shahidi wa Siri ufichuzi wa uhalifu unamwandama msaliti.
Hadithi hizi zinaakisi mada ya masuala mtambuko na maadili zinazompa msomaji na mwanafunzi hamu ya kujiburudisha, kasi ya kusoma, ari ya kujivinjari na uwezo wa kuwa na umilisi. Kupitia msururu huu wa hadithi, msamiati huongezeka, msamiati hupanuka na uzoefu wa mambo unaimarika.