- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- orders@storymojaafrica.co.ke
Je, unajua kuwa vitabu vya hadithi ni nyenzo za kimsingi katika ujifunzaji na ufundishaji wa lugha? Kusoma vitabu vya hadithi huchangamsha akili, huchochea ubunifu na kukuza fikra tunduizi. Ubunifu na fikra tunduizi ni baadhi ya umilisi wa kimsingi unaoendeleza ujifunzaji wa kudumu katika maisha ya mtu.
Shajara Yangu ya Usomaji: Kiwango cha 4 itakusaidia kuimarisha ujuzi wa lugha kwa kukupa maswali ainati ya fasihi, mada za majadiliano na shughuli za kiburudani ambazo zitakuza ari na mikakati yako ya kusoma na kuchambua matini. Kwa kutumia shajara hii, utajifunza kuwasiliana na kushirikiana vyema na wengine huku ukiboresha ujuzi wako wa msamiati na wa kufahamu matini.
Umepata mshirika wa kuaminika katika safari ya usomaji!