- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- orders@storymojaafrica.co.ke
Kalo, anayesomea mjini, anavumbua kinyago maalum chenye uwezo wa kutumia teknologia kuwafukuza tumbiri shambani. Baada ya uvumbuzi huu, wazazi wa Kalo wanahama kijiji ghafla. Haya yanayokea baada ya wageni fulani wa kiume kuwatembelea wazazi wa Kalo pale mjini. Kalo analazimika kuhama pamoja na wazazi kijijini. Nia yake ya kuwasilisha uvumbuzi wake katika kongamano la Kitaifa la Sayansi na Teknolojia inakumbwa na changamoto. Akiwa kijijini, Kalo anajipita katika hali tata. Je, ataweza kushiriki katika kongamano?
Fumbo la Wageni ni novela inayoangazia changamoto zinazowakabili wasichana wanaoishi katika bara la Afrika. Baadhi ya maudhui yaliyoshughulikiwa ni elimu, utamaduni wa ukeketaji wa wasichana na ndoa za mapema za wasichana.