- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- orders@storymojaafrica.co.ke
Hii ni hadithi kwa watoto wenye umri wa miaka 8-9 (Gredi 4).Ni kitabu kinachopambana na ufisadi na ushauri kwamba mwisho wa ufisadi huanza na wewe.
Jumatatu asubuhi, Malit ameshindwa kuamka ili aende shuleni. Dada yake mdogo, Nashipae, anashangazwa na kulala huku kwake kwa muda mrefu. Je, ni tabia mpya ya Malit ama anaugua? Kwa kawaida, Malit ndiye humwamsha Nashipae kila siku. Nashipae anawaarifu wazazi kisha wanatambua kuwa Malit anaugua. Anapelekwa hospitalini mbiombio. Bi Pulei anapomfikisha mwanawe Malit hospitalini, anagundua kuwa ufisadi umekita mizizi huko. Mama yuko katika njia panda. Atoe hongo ili mwanawe ahudumiwe ama asitoe ili adumishe uzalendo?