- +254 733 838 161 / +254 202 089595
- orders@storymojaafrica.co.ke
Tusome kwa Hatua ni kitabu kilichoandikwa kwa kuzingatia mbinu bora za ujifunzaji wa lugha kama ilivyoelekezwa katika mtaala wa shule ya chekechea. Kitabu hiki kinalenga kumwongoza mwanafunzi katika hatua za kusoma ambazo ni: kutambua herufi, kutamka sauti, kuunda na kusoma silabi na maneno na kusoma sentensi na vifungu vya maneno.
Kitabu hiki pia kinamwongoza mwanafunzi jinsi ya kusoma na kujibu maswali ya ufahamu katika kiwango hiki.
Yaliyomo katika kitabu:
• Mazoezi ya kusoma ya kusisimua.
• Michoro ya kuvutia inayoambatana na maneno yote mapya.
• Mifano ya matumizi ya maneno mapya katika sentensi.
• Vielelezo vya ufahamu wa kusikiliza na kusoma.
• Mazoezi ya kusoma ya kujitathmni.
• Orodha ya maneno ya kufanyia mazoezi ya kusoma.
• Mazoezi ya imla.
• Usawa wa jinsia umezingatiwa kupitia michoro na
maandishi.